WANAWAKE 751 KATI YA 869 WALIOKWENDA KUJIFUNGULIA HOSPITALI WILAYANI NGORONGORO KATI YA JANUARI HADI MACHI 2018,WALIKUWA WAMEKEKETWA.
Waandishi wa habari kutoka katika
redio tano za mikoa minne Arusha, Manyara, Dodoma na Mara ambayo inayoongoza
kwa ukeketaji,watendaji wa vijiji,viongozi wa kimila,viongozi wa dini,Mganga wa
jadi na maafisa ustawi wa jamii wamekutana katika warsha ya siku tatu
halmashauri ya wilaya Ngorongoro Mkoani Arusha kujadili kuhusu kampeni ya
kupambana na ukeketaji na ndoa za utotoni.
Katika wilaya ya Ngorongoro taarifa
za ukeketaji zinasikitisha kwa namna takwimu za awali zinavyoeleza kwani kwa
miaka mitatu tangu 2016 hadi 2018 ukeketaji unaongezeka badala ya
kupungua.
Mratibu wa huduma za Afya kwa Mama
na mtoto wilayani Ngorongoro Anna Masago amesema Kati ya wanawake 2991
waliofika hospitalini kwaajili ya huduma ya afya wakinamama 1783 ambayo ni
asilimia 66% wamegundulika kuwa wamekeketwa
Mwaka 2017 wanawake 2731 walioenda
hospitalini Kati yao 2201 waligundulika kukeketwa ambao sawa na asilimia 81% na
mwaka 2018 mwezi January hadi mach wanawake 869 Kati yao 751 sawa na asilimia
86% wamegundulika kukeketwa.
Kufuatia ripoti hiyo Mkurugenzi wa
halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Siumbu amesikitishwa na takwimu
hizo huku akieleza kuwa halmashauri yake ndiyo iko nyuma katika masuala ya
maendeleo huku akielezwa kuwa sababu inayopeleka Hali hiyo ni wakazi wa eneo
hilo kushikilia mila potofu.
source.triple a fm/arusha


Post a Comment