MAONESHO YA MIFUGO NA KONGAMANO LA WIKI YA MAZIWA YAANZA ARUSHA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqwaro amewataka wananchi
wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika kutembelea Maonesho ya
Mifugo na Kongamano la wiki ya maziwa katika viwanja
vya nanenane Njiro Mkoani hapa ili kuweza kupata elimu juu ya unywaji wa
maziwa na kujua teknolojia mbalimbali za ufugaji kwa lengo la kufuga
kwa tija.
Akiongea na waandishi wa habari Daqaro kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa Mkoa kwa kushirikiana na baraza la kilimo
taifa pamoja na bodi ya maziwa wameamdaa maonesho kitaifa ya kwanza ya
Mifugo na maadhimisho ya 21 wiki ya maziwa kwa lengo la kujenga ubia wa
kibiashara na mtandao.
Amefafanua kuwa malengo mengine ya Maonesho hayo ni
kubadishana ujuzi ,teknolojia na uzoefu, kutafuta fursa za masoko
miongoni mwa wadau pamoja na kuainisha fursa na kushawishi uwekezaji
katika sekta ya Mifug.
Source.triple a fm/arusha

Post a Comment