TANZANIA NI NCHI YA 9 KWA UCHANGIAJI MKUBWA WA ASKARI KATIKA ULINZI WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia
Siku ya leo na Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali ili
kuonesha mshikamano wake na watu wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kifo
na hali tete katika kuadhimisha miaka 70 ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa
Mataifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari
Bwana Guterres amesema kuwa umoja wa maifa unatoa shukrani kwa wanaume
na wanawake zaidi ya milioni moja ambao wametumika chini ya bendera ya
Umoja wa Mataifa kuokoa maisha ya watu wengi ikiwa ni pamoja na kuwaenzi
askari wenye kofia za samawati zaidi 3,700 ambao walipoteza maisha yao
katika miongo saba iliyopita.
Amefafanua kuwa wakati wa migogoro isiyoelezeka na
kuongezeka kwa vifo vya walinzi wa amani anatambua huduma ya kujitolea
duniani kote hivyo ameahidi kuchukua Hatua kwa ajili ya Walinzi wa
Amani kwa kufanya operesheni zao kuwa madhubuti na salama zaidi katika
mazingira ya sasa yenye changamoto.
Aidha atakaporejea kutoka Mali Bwana Getteres ataongoza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York siku ya Ijumaa, tarehe 1 Juni ambapo ataweka shada la maua kuwaenzi wale wote waliopoteza maisha yao katika huduma ya amani na pia ataongoza sherehe ya kutunuku Medali kwa watumishi 129 wa kijeshi, polisi na raia waliopoteza maisha yao katika operesheni za kulinda amani mwaka 2017 moiongoni mwao wakiwa walinzi 20 kutoka Tanzania.
Tanzania ni nchi ya 9 kwa uchangiaji mkubwa wa askari katika Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa ambapo hivi sasa inachangia karibu wanajeshi na polisi 2,700 kwenye operesheni za ulinzi wa amani huko Abyei, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lebanon, Sudan pamoja Sudan Kusini.

SOURCE.TRIPLE AFM/ARUSHA

Post a Comment