MAAFISA FEKI WA TAKUKURU WANASWA WAKIPOKEA RUSHWA IKULU
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa TAKUKURU mkoani Katavi imewakamata Nicodemo Peter na Peter Mwaninsawa wakazi wa Mtaa
wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Tshs 400,000
wakati wakiwa nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi baada ya kuijifanya
wao ni maafisa wa TAKUKURU.
Wahumiwa hao wawili walikamatwa wakiwa wanapokea kiasi hicho cha
fedha katika eneo la nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi iliyopo
jirani na ofisi ya TAKUKURU.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa
Katavi John Minyenya aliwaambia wandishi wa Habari ofisini kwake kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia mtego ulioandaliwa na taasisi hiyo baada ya
kuwa wamepata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita
ni maafisa wa TAKUKURU wa kitengo cha uchunguzi.
Alisema kabla ya kukamatwa kwa
wahumiwa hao walimpigia simu msiri wa TAKUKURU na kujitambulisha kuwa wao ni
maafisa wa TAKUKURU na wanalo jalada la uchunguzi za huhuma zinazomkabili msiri
huyo.
Watuhumiwa hao walimtaka awape kiasi
cha shilingi laki nne ili waweze kulifunga jalada kwa kufuta tuhuma
zilizomkabili msiri huyo ambae ni Mtendaji wa Kijiji cha Vikonge Wilayani
Tanganyika ambaye walidai kuwa alikuwa na tuhuma za kupokea rushwa ya kutoka
kwa wafugaji ambao alikamata mifugo ya wafugaji na kisha aliiachia baada ya
kupokea rushwa kiasi cha Tshs 2,500,000/= .
Minyenya alieleza kwa kuwa msiri
huyo ambaye hapendi na anapinga rushwa alilazimika kufika kwenye ofisi ya
Takukuru na kutoa taarifa juu ya maafisa hao bandia wa Takukuru .
Ndipo Takukuru walipoanza kufanya
uchunguzi juu ya malalamiko hayo kutokana na TAKUKURU kutokuwa na watu wenye
tabia kama hiyo ya kuomba na kupokea Rushwa.
Alisema ndipo hapo TAKUKURU
walipoandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walimtaka msiri huyo
awapelekee fedha hizo nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Katavi kwa kuwa ni jirani
na ofisi yao ya Takukuru ili iwe rahisi wao kutoka ndani ya osisi ya TAKUKURU
na kufika kwenye eneo la tukio.
Kufuatia makubaliano hayo msiri
ulipofika muda wa kupeleka fedha kwa maafisa hao bandia alikwenda kuchukua
fedha zilizokuwa na namba za TAKUKURU na kisha aliwapelekea kwenye eneo
walilokuwa wamekubaliana kwa ajiri ya kubabidhiana na mara tuu walipo pokea
fedha hizo nje ya jengo la Ikulu watuhumiwa hao walikamatwa na Maafisa wa
TAKUKURU huku wakiwa na fedha hizo.
Kamanda Minyenya alisema watuhumiwa
hao wanaendelea kushikiliwa na watafikishwa mahakamani ili wakaweze kujibu
mashita mawili ambayo ni kujifanya maafisa wa TAKUKURU na shitaka la pili
ni kuomba na kupokea rushwa.

Post a Comment