WAMAREKANI WASAIDIA KUKUZA TEHAMA ARUSHA DC




Shule 10 za sekondari kati 27 za halmashauri ya Arusha zimenufaika na mradi wa tehama kwa kupewa zaidi ya kompyuta 20 kwa kila shule zinazosaidia walimu katika kufundisha na wanafunzi kujifunza.

Mratibu wa mradi huo ambaye pia ni afisa tehama wa halmashauri hiyo David Nyangaka amesema kuwa kompyuta hizo zimetolewa na wafadhili kutoka Marekani na zimekuwa msaada mkubwa  katika elimu ndani ya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dokta  Wilson Charles Mahera amesema kuwa shirika  hilo limeahidi kuongeza kompyuta hizo kwa shule tatu  ambapo wamependekeza ziende  katika shule ya Kimnyak, Kiranyi na Sokon two.

Adam Namama Mwalimu wa kompyuta katika Sule ya sekondari  Mringa amesema kuwa shule yao ina  kompyuta 24 na wanazitumia kwa manufaa ya walimu na wanafunzi  ambapo wote kwa pamoja wanazitumia kwa kutafuta matirio ya masomo mbalimbali ya kujifunzia na kufundisha.

Mwanafunzi wa shule hiyo kutoka kidato cha pili na cha tatu Recho Aron, David Smoke na Floriana  Amedeus  wameeleza kuwa kompyuta hizo zinawasaidia kupata vitabu mbalimbali vinavyowasaidia kusoma vizuri ikiwa ni pamoja na kupata ujuzi utakao wasaidia baada ya kuhitimu.

Source.tripleafm habari  machi 04 2018

No comments

Powered by Blogger.