KONGAMANO LA BIBI NI NGUZO LAACHA GUMZO ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwira ametoa wito kwa
halmashauri zote hapa chini kuangalia uwezekano wa kuwapa wazee bima ya
afya pamoja na kuwapa kipaumbele katika mgao wa fedha za miradi ya
vijana na wanawake zinazotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Bi Mgwira ametoa wito huo Leo wakati akifunga Kongamano la
wabibi lililofanyika Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa maisha ya wabibi
wengi hayana akiba,malipo ya uzeeni wala fidia ya majanga hivyo
halmashauri ziwape kipaumbele.
Bibi Edith Tarimo mshiriki wa Kongamano hilo amesema kuwa
tangu virusi vya ukimwi viingie nchini wabibi wamekuwa wakiwalea watoto
wa watoto wao waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo ambapo bibi
mmoja analea wajukuu wanne hadi 10 jambo ambalo sio jepesi kwao.
Hata hivyo Kongamano hilo lililowashirikisha wabibi 250
kutoka Mkoa ya Tanzania na 40 kutoka nchi za nje umebeba kauli mbiu
isemayo "bibi ni nguzo" ambapo umehitimishwa kwa maandamano ya amani
yaliyoendanda sambamba na ubebaji wa mabango yanashinikiza kutengewa
Siku maalum ya wabibi nchini.
Source.tripleafm habari Machi 04 2018





Post a Comment