TASAF AWAMU YA TATU YAKUMBUSHWA KUWAFIKIA WALENGWA HALISI



Baadhi ya wazee kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wameilalamikia serikali juu ya mradi wa kunusuru kaya masikini Tasaf awamu ya Tatu kutokuwafikia watu Mwenye mahitaji maalum badala yake kuwafikia  watu wenye  nguvu za kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari bibi Christin Mahenga kutoka dar-es-saalam katika Kongamano la akina bibi lililofanyika Arusha amesema kuwa mradi huo umekuwa  ukiwafikia watu wanaoshindwa kujishughulisha kwasababu  ya uvivu na kuwaacha  wazee wasiojiweza bila msaada.

Jane Marigo bibi kutoka Arusha amesema pamoja na serikali kuwasaidia wazee kupata matibabu bure bado wanaiomba iwasaidie fedha za kujikimu kupitia mradi wa Tasaf ili waweze kuanzisha mradi itayowasaidia kuwaleo wajukuu walioachwa na wazazi wao kwa kufariki dunia na kupata lishe itayowaimarisha.

Kwa upande wake Tajiaeli Mahega mratibu wa Tasaf Jiji la Arusha amefafanua kuwa walengwa wanaohusika na malipo ya kaya masikini ni wale wanaoahindwa kupata Milo mitatu kwa Siku na vigezo vingine vinawekwa na wananchi katika maeneo yao.

Source.tripleafm habari machi 4 2018

No comments

Powered by Blogger.