BODABODA JENGENI HESHIMA YENU-MWIGULU
Waziri wa mambo ya ndani Dokta Mwigulu Nchemba amewataka
madereva bodaboda kote nchini kufanya kazi ya bodaboda kuwa ya heshma
kutokana na kazi hiyo kuleta maendeleo makubwa kwa nchi kwa kurahisisha
utoaji wa huduma na na upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Mwigulu ametoa wito huo wakati akizungumza na madereva
bodaboda Mkoani Arusha baada ya kusikiliza taarifa ya marejesho ya
mkopo wa pikipiki uliotolewa kwa madereva bodaboda wa kata 25 za wilaya
ya Arusha ambapo amesema kuwa;bodaboda ni hatua kubwa ya mafanikio ya
nchi hivyo wanapaswa kujivunia na kufanya shughuli ya heshima na sio
shughuli inayofanywa na watu waliokosa kazi za kufanya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
ameeleza kuwa walifikia utaratibu wa kutoa bodaboda miambili zenye
thamani ya millioni mianne baada ya kuona kuwa madereva bodaboda ni watu
ambao hawawezi kupata fursa za kukopa kwenye mabenki kutokana na
kutokidhi vigezo na masharti.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa madereva wa bodaboda Jiji la
Arusha (UBOJA) Bwana Maulid Makongoro ameeleza kuwa kwa sasa umoja huo
una wanachama elfu tano ambapo walipata fursa ya utatuzi wa changamoto
ya mitaji iliyokuwa ikiwakabili kwa kupata mkopo wa usio na riba wa
pikipiki mia Mbili kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Bwana Makongoro ameeleza pikipiki hizo ziligawanywa kwa
uwiano sawa kwa kata zote 25 za Jiji la Arusha ambapo kila kata
walipata pikipiki 8 na hadi sasa wamefanya marejesho ya zaidi ya
millioni mia tatu.
Source.tripleafm/habari machi 4 2018

Post a Comment