KAMATI ZA KUPINGA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO KUUNDWA KILA KATA ARUSHA DC
ARUSHA.
Mkurugenzi wa halmashauri ya arusha vijijini Dokta Charles Mahera ameiagiza Idara ya ustawi wa jamii kuhakikisha kamati zinazopinga ukatili kwa wanawake na watoto yanaundwa katika kata zote za halmashauri hiyo.
Dokta Mahera amesema hayo Leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani katika halmashauri hiyo ambapo ameeleza kuwa kamati hizo zitasaidia kutokomeza unyanyasaji na kutokomeza mila potofu pamoja na mimba za utotoni.
Hindu Ally Mbwega Mkurugenzi wa kituo cha maendeleo ya wanawake,watoto na Vijana amesema kuwa unyanyasaji wa wanawake na watoto umekuwa ni mwingi kupita kiasi kutokakana na mambo mengi kufanyika kichinichini hasa maeneo ya pembezoni ikiwa ni pamoja na haki kupotelea mahakamani.
source.triple a fm habari-machi 8 2018

Post a Comment