MAWIFI ACHENI TABIA YA KUNYANYASA WAJANE-MKUU WA WILAYA
ARUSHA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini GabrieL Daqaro amewataka mawifi kuacha
tabia ya kuwanyanyasa wajane na kuwanyang”anya mali walizoachiwa na
waume zao ili kupunguza migogoro katika familia.
Mh Daqaro ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya
Siku ya wanawake duniani yalioadhimishwa katika jiji la Arusha ambapo
wanawake zaidi ya 700 wameshiriki katika sherehe hizo.
Amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi kwenye ofisi za serikali
kuhusu wanawake waliofiwa na waume zao baada ya hapo wanapata
manyanyaso baada ya kuachiwa mali za urithi.
Mkuu huyo amewataka ndugu wa mume baadhi kuacha tabia hiyo na kutambua
kuwa mali zinazaochwa na mume ni kwa ajili ya watoto na watengeneze
upendo baina yao kwa kuwa wengi wamekuwa hawapendani wao kwa wao.
Daqaro amewasisitiza wanawake kuendelea kupiga kelele ili kupinga
vitendo vya kikatili na ubakaji kwa kuwa viendo hivyo bado vipo bado
kwenye jamii.
Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha amesema kuwa kama jiji wamejidhatiti
katika kutoa mikopo ya wanawake ambapo wanategemea kutoa mikopo ya
wanawake shilingi bilioni 2
SOURCE.TRIPLE A FM HABARI-MACHI 8 2018

Post a Comment