SOKONI TWO ARUSHA WAFANYA HARAMBEE ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI







ARUSHA

Wananchi wa Kijiji cha Sokoni Two Kata ya Sokon Two katika Halmashauri ya Arusha wamefanya harambee kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji katika kijiji chao.

Bi Miriam Mosesi ambaye ni mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa endapo watafanikiwa kutatua changamoto hiyo itawawezesha akina mama kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwani muda mrefu wanautumia kutafuta maji.

Ka upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Obedi Melami amesema kijiji hicho chenye vitongoji vitano kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maji kutoka na maji wanayoyapata kutoka kijiji cha jirani kuhujumiwa na watu wenye mashamba makubwa.

Naye OLTESH Thobias ambaye ni mkazi wa kijiji hicho amesema changamoto kubwa inayosababisha maji yasifike katika kijiji hicho ni miundombinu; hivyo wameweza kupata zaidi ya milioni saba zitakazowezesha kuboresha miundombinu hiyo ili maji yapatikane.


Akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza; hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema serikali kupitia Kampeni ya Rais Dokta John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Source.tripleafm news/27.02.2018

No comments

Powered by Blogger.