MPANGO WA KUWAWEZESHA WAZEE KUPATA HUDUMA ZA AFYA BURE UPO PALEPALE-RC GAMBO








ARUSHA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali ina mpango kuwatambua wazee wote nchini ili waweze kupata vitambulisho vitakavyowasaidia kupata huduma za afya kwa kadri sheria, taratibu na sera za nchi zitakavyo ruhusu.

Gambo amesema hayo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la tatu Afrika la Akinabibi wanaolea wajukuu ambao wazazi wao wamefariki dunia ambapo ameeleza kuwa mpango huo utawasaidia kupata takwimu sahihi za akinabibi hao katika ngazi ya kijiji hadi mkoa ili kuweza kupeleka huduma mbalimbali kwao ikiwemo huduma ya afya.

Kwa upande wake Ndinini Kimesera mkurugenzi wa shirika linalojishughulisha na masuala ya maendeleo ya wanawake wa kimasai(MWEDO) amesema lengo kubwa la kongamano hilo ni kutambua nafasi ya bibi katika janga la Ukimwi hasa kwa kuwalea na kuwatunza wajukuu wao walioachwa na wazazi wao.

Christina David bibi kutoka Kimara jijini Dar-es-salaam ameeleza kuwa pamoja na serikali kuwaletea huduma ya elimu bure bado wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kuwalea wajuu kwa kushindwa kuwatimizia mahitaji mengine kama vile matibabu, sare za shule, madaftari pamoja na huduma nyingine muhimu.

Source.triplea fm habari/27.02.2018

No comments

Powered by Blogger.