“Kuna miradi viporo vingi sana katika Halmashauri zetu" WAZIRI JAFO
NTEGHENJWA HOSSEAH, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewataka viongozi wa Halmashauri zote Nchini kupitia
mipango iliyopo (Review) na
kupanga Upya Kimkakati miradi yote ya maendeleo
inayotekelezwa kwa Fedha za mfuko wa
Maendeleo ya Serikali Mitaa (LGDG).
Waziri Jafo ameyasema hayo kwenye Kikao Kazi cha kujadili
Mpango wa Utekelezaji wa
Miradi ya LGDG iliyoboreshwa kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
kilichohusisha baadhi ya
Wah. Wabunge, Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi
wa Mamlaka za Serikali
za Mitaa pamoja na Maafisa Mipango kilichofanyika katika
chuo cha Mipango kilichopo mjini
Dodoma.
Waziri Jafo alisema kuwa Bajeti ya Mfuko wa Maendeleo ya
Serikali za Mitaa kwa mwaka
huu wa Fedha ni Bil.251 ambazo hugawanywa kwa halmashauri
zote Nchini. Fedha hizi ni
nyingi sana na zinatosha kutekeleza miradi michache yenye
Tija na itakayopunguza
changamoto kwa wananchi wetu lakini kinachofanyika ni kuwa
halmashauri hugawanya
kiasi wanachopata kwenye miradi mingi ambapo sio rahisi
kuona matokeo kwakuwa miradi
mingi haikamiliki.
“Katika Halmashauri nyingi badala ya kugawanya Fedha hizi za
Ruzuku kwenye miradi mingi
kwa viwango kidogo kidogo ni vyema sasa tukajieleza kwenye
miradi michahe ambayo
tutahakikisha inakamilika kwa mwaka wa Fedha husika na
kuanza kutoa huduma kwa jamii”
Alisema Jafo.
“Kuna miradi viporo mingi sana katika Halmashauri zetu
ukiangalia Sekta ya Afya utakutana
Maboma mengi ambayo yangekamilika yangetumika kama Zahanati
au Vituo vya Afya,
Elimu utashuhudia magofu ya kutosha ambayo yangekamilika
yangetumika kama vyumba
vya madarasa hii yote ni kutokana na kupanga miradi mingi
kwa wakati mmoja sasa kwa
mwaka huu na kupitia Kikao hiki mfanye mapitio Upya na
mpange miradi michache
itakayokamilika kupitia bajeti kwa mwaka huu” Aliongeza
Jafo.
Waziri Jafo alisisitiza kuwa Katika Bajeti ya LGDG mwaka huu
Bil.66 zimeelekezwa kwenye
Sekta ya Afya nataka mkazisimaie mkakamilishe Maboma yaliyotelekezwa
kwa kipindi kirefu
na yakamilke tayari kwa kutoa huduma halkadhalika katika
maeneo mengine yote ambayo
Fedha hizi zitatumika.
Waziri Jafo alimalizia kuwa kikao hiki sio Semina wala eneo
la mapumziko kwa viongozi wa
halmashauri bali ni Kikao kazi hivyo Kitumike kama fursa
adhimu na muhimu ya kufanya
Mapitio ya Mipango ya halmashauri ambayo ikitekelezwa
italeta matokeo Chanya na
kuwapunguzia adha wananchi wetu.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI
Mhandishi Musa Iyombe
amesema Kikao hiki ni Maalumu kwa Viongozi wote ambao
wanahusika moja kwa moja na
kuwaletea wananchi maendeleo ili kwa pamoja tukubaliane,
tushauriane na tuelekezane
namna bora ya kutekeleza miradi hiyo ambayo inaonekana eneo
la Mipango halijafanyiwa
kazi kikamilifu.
“Viongozi wenzangu lazima suala la mipango liangaliwe kwa
Makini katika Halmashauri
zetu, Jambo hili lisipofanyika kwa Umakini lina madhara
makubwa kwa Jamii, litaturudisha
nyuma kimaendeleo na kila siku tutaona hatufanikiwa katika
miradi yetu kwa sababu tu
tulikosa umakini katika kuandaa Mipango yetu, hebu tupitie
upya mipango yetu na
tuhakikishe tunamaliza mradi mmoja kwanza kabla ya kuanza
mwingine” alisema Mhandisi
Iyombe.
Akizungumza na wajumbe wa Kikao kazi Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-Menejiment ya Utumishi
wa umma na Utawala bora Dkt.Laurean Ndumbaro amewakumbusha
watumishi wote
kufanya kazi kwa kuzingatia Hotuba ya Mhe.Rais Dkt. John
Joseph Pombe Magufuli
alipohutubia Bunge na kusisitiza Uwajibikaji, Utumishi wa Umma
unaojali misingi ya
Uadilifu, Weledi wa Kitaaluma, Maadili na Uadilifu katika
Utendaji kazi wetu.
“Watumishi wanapaswa kuwajibika kwa Serikali iliyopo
Madarakani kwa kutekeleza yale
yote yanayowapasa kutekeleza kwa mujibu wa miongozo kwa
watumishi wenzetu
tunaofanya nao kazi na kwa wananchi tunaowatumikia, tuwape
haki yao ya msingi ya
kuwahudumia na kuwalete maendeleo.” Alisema Dkt. Ndumbaro.
Kupitia Kikao hiki washiriki kutoka katika Halmashauri zote
watapitia Upya miradi ya
maendeleo waliyopanga kutekeleza kupitia Fedha za “LGDG” kwa
kuzingatia maelekezo
watakayopewa kabla ya kupokea Fedha hizo kwa ajili ya
utekelezaji.
Post a Comment