BAADHI YA KAYA ZAONA MANUFAA YA TASAF AWAMU YA TATU ARUSHA







ARUSHA.

Baadhi ya wanufaika wa mradi wa TASAF awamu ya Tatu jijini Arusha wameishukuru serikali kwa kuwaletea mpango huo kwani umewasaidia kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila siku.

Wanufaika hao wametoa shukrani zao kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa CCM, Humphrey Polepole aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya TASAF ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Wamesema mradi huo umebadilisha maisha yao tofauti na awali kwani kwa sasa wanawezan kupata milo mitatu kwa siku, watoto kwenda shule, pamoja na kufanya biashara mbalimbali zinazowaingizia kipato.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbli ya TASAF Mratibu wa TASAF jiji la Arusha Tajiel Mahega amesema asilimia kubwa ya kaya maskini hizo tayari wamesha patiwa kadi kwa ajili ya matibabu (Tika) yenye uwezo wa kuhudumia kaya sita kwa kadi moja.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa CCM, Humphrey Polepole ameagiza wasimamizi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zenye upungufu wa chakula TASAF mkoa wa Arusha kufanya tathmini na kuongeza ruzuku kaya zinazofanya maendeleo ili kuongeza uzalishaji ili kuwa chachu ya maendeleo katika jamii.

Source.triple a fm habari/27.02.2018

No comments

Powered by Blogger.