"HARAKISHENI MRADI WA MAJI WA WB TUPATE MAJI"WANANCHI LIKAMBA
ARUSHA.
Wananchi wa kata ya Musa kijiji cha Likamba Wilayani
Arumeru wameiomba serikali kuharakisha utekelezaji wa mradi wa maji wa benki ya
dunia uliosimama kwa muda mrefu ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama
kwani hutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya shughuli za maendeleo.
Bi Evaline Abel mkazi wa kitongoji cha Olomponi amesema
tatizo la ukosefu wa maji limewafanya wanawake katika kata hiyo kushindwa
kufanya shughuli za maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji na
mara nyingine watoto hawaendi shule
Samwel Satian mkazi wa kitongoji cha Olomishira ameeleza kuwa wamekuwa
wakifuatilia utekelezaji wa mradi huo katika ngazi mbalimbali za wilaya hiyo
lakini bado hakuna kunachoendelea hali inayowanyima kuchangamkia fursa za
maendeleo zilizopo katika kilimo na ufugaji.
Akizungumzia kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo
Diwani wa kata hiyo Bi Flora Zelote amesema unatekelezwa katika vijiji vitatu
na katika kijiji cha Likamba umekamilika kwa asilimia 60.
Utekelezwaji mradi huo ulianza toka mwaka 2013 lakini
mpaka sasa bado haujakamilika; huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa maji.
sOURCE.TRIPLEA FM HABARI/27.02.2018

Post a Comment