SERIKALI YAOMBWA KUSIKIA KILIO CHA HUDUMA DUNI ZA AFYA OLDONYO SAMBU






ARUSHA.

Kufuatia kukabiliwa na changamoto za Afya ikiwemo ukosefu wa Wauguzi katika zahanati ya Oldonyo Sambu,pamoja na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya wananchi katika kijiji cha Oldonyo Sambu  Wilaya  ya Arusha wameiomba serikali kusikia kilio kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

Wakizungumza na triple A fm baadhi ya akina mama hao waliofika kupata huduma katika zahanati hiyo wamesema haina vifaa tiba vya kutosha na pia ina muuguzi mmoja hivyo kushindwa kuhudumia wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.

Wamesema umbali mrefu umekuwa ukisababisha adha kubwa hususani kwa akina mama wajawazito pindi wanapotaka kuhudhuria clinic kwa wakati na hata kina mama wengine hushikwa na uchungu wakiwa njiani kwenda kujifungua 

Bwana Piniely Meyasi amesema Zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa majengo,umeme  pamoja na  maji safi na salama hivyo ameiomba serikali  kutatua changamoto hizo mapema ili kuzuia athari zisiendelee kujitokeza 

Muuguzi wa zahanati hiyo ambaye  amekataa kutaja jina lake amekiri kuwepo kwa changamoto hizo  katika zahanati hiyo na kusema inategemewa sana  kwani  asilimia 80 ya wakazi wa kijiji  hicho na vijiji vya jirani  wanapatiwa huduma za afya hapo.

Pamoja na jitihada za serikali kupitia sekta ya afya kuwasisitiza akina mama wajawazito kuhudhuria clinic kwa wakati na kutojifungulia majumbani baadhi ya maeneo ya pembezoni utekelezaji wake bado ni changamoto. 

Source.triple a fm habari/27.02.2018

No comments

Powered by Blogger.