Takukuru yatia kapuni ushahidi wa Nassari na Lema
Takukuru yautupa ushahidi wa video wa wabunge wa Chadema, Joshua
Nassari na Godbless Lema ukiwaonyesha madiwani wa chama hicho waliohamia CCM
wakihongwa rushwa.
Madai hayo yametupiliwa mbali kwa kile kilichodaiwa kuwa
wabunge hao waliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo
hilo.
Imeeleza wabunge hao waliingilia uchunguzi na kuuvuruga ila
hawawezi kusema ni jambo gani walivuruga kwa sababu mambo mengine ni ya
kiuchunguzi.
Hivyo Takukuru imeamua kutupilia mbali ushahidi huo wa video
uliowasilishwa kwa flash na wabunge hao wa Chadema kwa kudai kuwa kuna kanuni
za utoaji wa ushahidi, video kama zilivyo haziwezi kuwa ushahidi tosha.
‘’Ile ni taarifa na ushahidi ni tofauti’’ amesema Musa Msalaba
ambaye ni msemaji wa Takukuru.
‘Ni kweli flash tulikabidhiwa lakini Nassari na wenzake kwa
sababu walivuruga uchunguzi hatuwezi kuendelea kufanya siasa kwa sababu ya
uchunguzi lazima uwe huru,;; amesema Msalaba.
Hata hivyo amesema kuwa kutokana na teknolojia kuwa kubwa zama
hizi mtu anaweza kuzichezea na kutengeneza kitu kama hiko na kikaonekana kweli.

Post a Comment