KINANA ATEULIWA TENA KUWA KATIBU MKUU.
Katibu mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa na
Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli kuendelea kuwa
katika nafasi yake kwa kipindi kingine.
Akiongea katika mkutano wa 9 wa
Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma amemshukuru kwa kazi yake
nzuri kwa muda wote ambao amekuwa katika nafasi hiyo huku
akiweka wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi kwasababu ameridhishwa na
utendaji wake wa kazi.
''Namshukuru ndugu Kinana kwa msaada
wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri anafaa
kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema Magufuli.
Kauli ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana
ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa
haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.
Baada ya kupata
nafasi hiyo Abdulrahman Kinana amemshukuru Rais Magufuli kwa
kumuamini pamoja na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kukijenga
chama hicho pamoja na nchi kwa ujumla.
Kinana aliwahi kuwa mtumishi wa
Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la
Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006, amechaguliwa kuwa Katibu mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.

Post a Comment