Raisi Magufuli amshukuru Raisi Mstaafu Kikwete
Mwenyekiti wa CCM Taifa,
Dkt. John Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoangalia
rushwa wala urafiki pindi alipomchagua kugombea urais na kutaka wanachama wake
kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu wenye mapenzi ya dhati na chama.
Dkt. Magufuli ameonya hayo
wakati akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo ambapo
amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa na kwamba kama Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete angeangalia hayo basi yeye asingepata nafasi alonayo
“Msichague watu kwa urafiki au
kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye
hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,”
amesema.
Aidha Dkt. Magufuli amewataka
wanachama wa chama chake kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa
ndani wa chama hicho.
“Vunjeni makundi chaguzi
zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye
kuendeleza makundi,” amesema
Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameweka
wazi hatosita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu
iwapo itabainika rushwa imetumika.

Post a Comment