AJALI YA COASTER,LORI YAUA WATANO MWANZA
Watu watano wamefariki
dunia na 13 wajeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya
Mwanza kwenda Shinyanga eneo la mtaa wa Buhongwa Nyamagana mkoa wa Mwanza baada
ya gari yenye namba za usajili T.107 BKK Toyota coaster kugongana na Lori.
Gari hiyo aina ya
Coaster ilikuwa ikiiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Badru Habibu
(33) mkazi wa Nyegezi na chanzo cha ajali hiyo kimefahamika kuwa ni mwendokasi
wa dereva wa Coaster aliyekuwa akijaribu kuyapita magari ya mbele bila
tahadhari na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 13.
Marehemu waliofariki
katika ajali hiyo hadi sasa ametambulika jina moja tu ambaye ni 1. Abdul
Mustafa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 42 hadi 45, huku marehemu
wengine wa nne majina yao bado hayajafahamika.
Aidha majeruhi wote
kumi na tatu wapo hospitali ya rufaa ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao
zinaendelea vizuri, miili ya marehemu pia imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya
Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi, Ahmed Msangi anatoa wito kwa waendeshaji
wa vyombo vya moto hususani madereva wa magari ya abiria akiwataka kuwa makini
pindi wawapo barabarani huku wakijua wamebeba roho za watu, hivyo wazingatie
sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi
ya aina kama hii yanavyoweza kuepukika.

Post a Comment