WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI WAAPISHWA

Wabunge 54 wa bunge la jumuiya ya Afrika mashariki leo wameapishwa rasmi kuwa wabunge wa jumuiya hiyo ili kuweza kuwakilisha nchi zao katika bunge hilo katika kutatua masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Kwa kawaida bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki huongozwa katika kipindi cha miaka mitano kwa wabunge na kisha kufanyika uchaguzi wa kuwateua wabunge wa wawakilishi kutoka katika nchi tano ikiwemo Uganda,Rwanda,Kenya,Tanzania na Burundi ambapo nchi ya South Sudan kwa mara ya kwanza ndiyo inaingia katika bunge la jumuiya baada ya wakuu wan chi kukubaliana mwaka jana kuwa South Sudan kuwa katika umoja wan chi za afrika mashariki.

Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika mashariki kutoka nchini Tanzania wakapata wasaa wakuelezea namna walivyojipanga katika kuhakikisha wanawapa wananchi wa jumuiya ya Afrika Masharikikipaumbele katika kutatua changamoto zao.

Baadhi ya wabunge kutoka South Sudan ,Kenya na Uganda wanasema kuwa ni jukumu lao kuhakikisha wanaweka sawa mambo ya soko la pamoja pamoja na mambo mengine wanawakilisha nchi zao hivyo ni vyema kama kila mmoja akajiandaa kutimiza wajibu wake katika bunge hilo ambalo wengi ni vijana.

Lakini kama nchi ya Tanzania kwa niaba ya spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu ambaye ni mwenyekiti wa bunge la Tanzania anasema kuwa wana hari kubwa na bunge hilo na kwamba wabunge wasijiingize katika makundi ya ushabiki na badala yake wafanye kazi kwa maadili ili kufanikiwa katika shughuli zao za kibunge.

Hata hivyo katika zoezi hilo la viapo kwa wabunge hao limeambatana na uchaguzi wa spika ambao utafanyika hapo baadae na kwamba wanatarajia bunge hilo kuongozwa na spika wa Tanzania Adam Kimbisa.

No comments

Powered by Blogger.