KUNA MAWAKILI WENGI MIJINI WAKATI VIJIJINI WANANCHI WAKIKOSA MSAADA WA KISHERIA-JAJI MKUU
ARUSHA.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahimu Hamis Juma Amewataka Watendaji wa Mahakama Kote Nchini kuhakikisha Wanatoa Nakala za Hukumu kwa Wakati ili Kuondoa Adha kubwa ya Wananchi wanaokufatilia Kesi Mahakamani.
Akizungumza Katika kikao cha Menijementi ya Mahakama kilichofanyika Mkoani Arusha na kukutanisha watumishi ngazi za Mahakama za wilaya 52 kutoka kanda ya kusini, kaskazini, kati lengo likiwa ni kufanya Tathimini ya Mpango mikakati ya Miaka 5 Ijayo.
Profesa Ibrahimu amesema ni muhimu kwa Watendaji wa Mahakama Kufanya Tathimini ya Mipango kazi pamoja na uwepo wa mikakati Thabiti itakayo weza kujenga mfumo imara na kuondokana na uwepo wa makosa madogo madogo ambayo yanasababisha udhaifu ,Jambo ambalo amewataka Majaji na Mahakimu wakati wa usikilizaji wa mashauri Mbalimbal kutoa Hukumu kwa wakati .
Pia ameongeza kuwa kumekuwepo na mawakili wengi mijiini jambo ambalo Wananchi waliopo vijiijini wanashindwa kupata msaada nakusisitiza kuwa ni vyema kukawepo na Usawa pande Zote ili kufanikisha Huduma na kuongeza hari ya kuwatumikia Wananchi.
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga amesema Mahakama inajukumu la kufanya maboresho katika utendaji kazi wake lengo likiwa nikufanya maboresho Katika Mahakama za mwanzo na kutoa haki na ufumbuzi Katika maeneo machache na kurudisha Imani ya Wananchi kuiamin Mahakama.
Kwa Upande wake Mkuu wa kitengo cha maboresho Zahara Maruma amesema malengo ya maboresho Kwa mwaka 2020_2025 ni kuhakikisha wanayafikia maeneo 17 ya Mipango mikakati waliyojiwekea na kutimiza Nguzo ya Utawala bora na namna ya kuboresha Mifumo ya Taasisi zakimahakama kama Dira ya Utoaji wa haki sawa kwa Watu wote.
source.tripleafm habari-machi 8 2018

Post a Comment