KWA MARA YA KWANZA KITUO CHA AFYA KALOLENI CHAFANYA UPASUAJI
ARUSHA.
Wananchi katika mkoa wa Arusha ambao wamekuwa wakitegemea zaidi vituo vya afya vilivyopo katika maeneo yao kupata huduma za afya;hivi sasa wataanza kupata huduma za kitabibu za upasuaji katika vituo hivyo.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Onanch Timoth amesema ifikapo Julai mwaka huu , vituo vya afya saba katika Mkoa wa Arusha vitakuwa na Huduma ya Upasuaji ili kuepusha mrundikano wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha maarufu kama MOUNT MERU.
Dokta Onach amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Huduma hiyo ya Upasuaji iliyofanyika kwa mara ya kwanza katika kituo cha afya cha Kaloleni ambapo kitakuwa na uwezo wakuhudumia watu zaidi ya wanne.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa masuala ya Upasuaji kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha Dokta Ngeta Semba ;amesema hiyo ni hatua nzuri kwakuwa wametekeleza agizo la Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu la kila kituo kuwa na huduma ya upasuaji.
Kabla ya hatua hii,vituo mbalimbali vya afya na zahanati katika mkoa wa Arusha vilikuwa havina huduma ya upasuaji hali ambayo ilikuwa inawalazimu wagonjwa kupelekwa hospitali ya mkoa au katika hospitali binafsi,kupata huduma hiyo muhimu,na kusababisha msongamano katika hospitali hizo na gharama.
Source.tripleafm habari 20.02.2018
Post a Comment