Mkurugenzi aibuka kidedea kura za maoni Jimbo la Nyalandu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Joseph Monko ameshinda kura ya maoni CCM katika jimbo la Singida Kaskazini, baada ya kuzoa kura 21 kati ya 112 zilizopigwa
Monko amepata ushindi katika uchaguzi uliofanyika katika Kijiji cha Ilongero wilayani Singida, ukiwa ni
wa marudio baada ya CCM kufuta mchakato wa awali kutokana na kuwepo tuhuma za
rushwa
Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo katibu
msaidizi wa idara ya oganaizesheni ya makao makuu CCM, Steven Kazindi
amesema nafasi ya pili imechukuliwa na Choyo Japhet aliyepata kura 20 na
mshindi wa tatu ni Manase Maghina
Uchaguzi huo umeshirikisha wagombea 22 walijitokeza kuomba
kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la
Singida Kaskazini
Awali, uchaguzi ulifanyika Desemba 10,2017 ambao ulifutwa na
vikao vya ngazi ya juu ya CCM ikilezwa uligubikwa na vitendo vya rushwa
Kazindi amesema kura ya maoni haiteui mgombea isipokuwa
inatumika kupima nani atauzika
“Vikao vyenye mamlaka ndivyo vyenye dhamana ya kuteua mwana
CCM atakayekidhi vigezo vinavyohitajika katika uchaguzi,” amesema
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi katika
jimbo hilo utafanyika Januari 13,2018
Jimbo la Singida Kaskazini lipo wazi baada ya Lazaro
Nyalandu kujivua ubunge alioshinda akiwa CCM na kuhamia Chadema.

Post a Comment