BREAKING: Askari Magereza Arusha amuua askari mwenzie kwa risasi
Polisi inamshikilia kwa mahojiano askari Magereza wa Gereza
la Kisongo jijini Arusha, Koplo Faustine Masanja kwa tuhuma za kumuua mwenzake
wakiwa kazini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo
amethibitisha tukio hilo lililotokea leo Alhamisi Desemba 14,2017 asubuhi
Amesema baada ya Masanja kumjeruhi mwenzake Koplo Ombeni kwa
risasi, alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ambako alifariki dunia
Kamanda Mkumbo ameahidi kutoa taarifa zaidi baada ya
uchunguzi kukamilika ili kubaini chanzo na sababu za tukio hilo
Hata hivyo, taarifa zinadai huenda chanzo cha shambulio hilo
kikawa ni wivu wa mapenzi

Post a Comment