Benevento wavunja rekodi ya Manchester United

Klabu ya Benevento nchini Italia imevunja rekodi ya Manchester United ya kuwa klabu iliyoanza msimu vibaya zaidi katika ligi mojawapo kati ya ligi tano kuu za soka Ulaya.

Hii ni baada ya klabu hiyo kulazwa 2-1 muda wa ziada na Sassuolo.

Limbukeni hao wa Serie A wameshindwa mechi zao 13 za kwanza kwenye msimu na hivyo wakavunja rekodi ya United ambao walishindwa mechi 12 mwanzo wa msimu wa 1930-31.

Alessandro Matri aliwaweka Sassuolo kifua mbele lakini Samuel Armenteros akasawazisha kabla ya Gaetano Letizia alioneshwa kadi nyekundu upande wa Benevento.

Domenico Berardi alipoteza penalti upande wa Sassuolo kabla ya Federico Peluso kuwafungia bao la ushindi.

Benevento, ambao walifanikiwa kurejea Serie A mtawalia, walidhani wangepata alama yao ya kwanza ya msimu pale mkwaju wa penalti wa Berardi ulipogonga mwamba na kukosa kuingia.

No comments

Powered by Blogger.