“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria-WAZIRI MKUU
MASASI.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali
imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana
tunawataka
watoe taarifa za watu wanaotaka kuwakwamisha kimasomo kwa watendaji wa vijiji
kwenye maeneo yao.
Alitoa agizo hilo Jumatatu, Februari 26,
2018 wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa wilaya ya Masasi
akiwa katika siku ya kwanza ya ziara
yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Waziri Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika
jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na
atakayebainika kukatisha masomo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema Serikali itatoa
adhabu kali ya kifungo cha miaka 30
jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa
kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya
wageni.
“Tukikukuta na binti wa shule katika kona
isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti
wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”
Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi
watakaowaozesha watoto kike ambao bado wanafunzi na kwa upande wa wazazi
watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za
kisheria.

Post a Comment