SERIKALI YA AWAMU YA TANO INADHAMIRA YA DHATI KUHAKIKISHA HUDUMA YA MAJI INAWAFIKIA WOTE-MAKAMU WA RAIS SAMIA
Makamu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameendelea na
ziara yake katika mkoa wa Simiyu ambapo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa
ujenzi wa bwawa la maji kwa ajili ya binadamu na mifugo katika eneo la
Mwanjolo, wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Bwawa
hilo la maji litahudumia wananchi kumi na tatu elfu na mifugo laki moja na elfu
nane wa Mwanjolo, mradi huo mpaka kukamilika utatumia shilingi za kitanzania
bilioni 1.6 na utahifadhi kiasi cha maji lita 345,129,000.
Makamu
wa Rais aliwataka wananchi wa Mwanjolo kulinda vyanzo vya maji na kutunza
mazingira.
Akizungumza
na Wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji jiwe hilo la msingi Makamu wa Rais
alisema “ Serikali ya awamu ya tano ina
dhamira ya dhati ya kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi wote”
Makamu
wa Rais aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa kulima pamba kwa wingi
ambapo wilaya hiyo inategemea kilo 84 na kuwaahidi wananchi hao kuwa dawa za
kuulia wadudu zitapatikana kwa wingi kuanzia mwisho wa mwezi huu kwani serikali
imetoa fedha zaidi ya bilioni 9
Makamu
wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa barabara zote ambazo ilani ya uchaguzi
imeahidi kuzijenga zitajengwa na zile ambazo hazipo kwenye ilani ila zina
umuhimu zitaingizwa kwenye bajeti ijayo.
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kisesa
Mhe. Luaga Mpina alisema kuwa kati ya kata 13 ni vijiji vine tu vina maji hivyo
alimuomba Waziri wa Maji kusaidia zaidi upatikanaji wa maji.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe aliahidi kusimamia kwa ukamilifu
upatikanaji wa maji .
source.vpo-tripleafm-20.02.2018



Post a Comment