OKWI AING'ARISHA SIMBA DJIBOUT SASA KUKUTANA WAARABU





SIMBA SC imesonga mbele Raundi ya Kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Gendarmerie Tnare ya Djibouti baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo mjini Djibouti City.
 
Katika mchezo wa leo uliofanyika Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled, bao pekee la ushindi la Simba limefungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 55.
 
Kwa kuunganisha na ushindi wa 4-0 kwenye mechi ya kwanza jumapili ya wiki iliyopita, Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa 5-0 na sasa itakutana na El Masry ya Misri iliyoitoa Green Buffaloes ya Zambia. 

Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yussuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, James Kotei, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi na Muzamil Yassin.

source.tripleafm-supersports-20.02.2018

No comments

Powered by Blogger.